Mahakama yamfuata Manji hospitali, asomewa mashtaka ya uhujumu uchumi

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imelazimika kuhamishia shughuli zake katika Hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa muda kumsomea mfanyabiashara Yusufali Manji (41), mashitaka ya uhujumu uchumi yanayomkabili. Manji amesomewa mashtaka hayo katika Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo Hospitalini hapo mbele ya Hakimu Mkazi Mhe. Huduma Shaidi. Katika kesi hiyo, Manji anashitakiwa pamoja na wenzake watatu, Meneja Rasilimali ...

Soma Zaidi

Rais Magufuli atoa agizo la kusitisha utoaji wa leseni za kuchimba madini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo ameiagiza Wizara ya Nishati na Madini kusitisha utoaji wa leseni mpya za uchimbaji na halikadhalika leseni ambazo zimeisha muda wake. Ametoa maagizo hayo alipokuwa akizungumza na wananchi wa Geita ambao walizuia msafara wake katika maeneo mbalimbali wakati akiwa njiani kuelekea Chato. Mapema kabla, Mheshimiwa Rais alihitimisha ziara ...

Soma Zaidi

Nyota tegemezi wa Chelsea atimkia Aston Villa

Aston Villa wamemsajili aliyekuwa mchezaji wa Chelsea na nahodha wa timu ya Uingereza John Terry. Beki huyo mwenye umri wa miaka 36 ambaye kandarasi yake katika uwanja wa Stamford Bridge ilikuwa imekwisha mnamo tarehe 30 mwezi Juni ametia saini kandarasa ya mwaka mmoja na klabu hiyo ya ligi ya mabingwa. Terry alisema kuwa alikataa maombi ya kuendelea kucheza katika ligi ...

Soma Zaidi

Korea Kaskazini yarusha kombora katika bahari ya Japan

Korea Kaskazini imerusha kombora jingine la masafa marefu kutoka jimbo lake la magharibi kulingana na mamlaka ya Japan na Korea Kusini. Kombora hilo lilirushwa kutoka Bangyon Kaskazini mwa mkoa wa Pyongan kulingana na chombo cha habari cha Yonhap kikitaja duru za jeshi la Korea kusini. Tokyo imesema kuwa kombora hilo huenda lilianguka katika eneo la kiuchumi la bahari ya Japan. ...

Soma Zaidi

Cheki basi la Singida UTD

Singida United iliyopanda daraja msimu huu imeendelea kuonyesha kuwa inataka kuwa moja ya klabu za mfano hapa nchini hii ni baada ya leo Jumatatu kutambulisha basi lao jipya ambalo itakuwa ikilitumia kwa safari zake mbalimbali za michezo ya ligi kuu bara na ile ya kombe la shirikisho. Utambulisho wa basi hilo lenye thamani ya Shilingi Milioni 330 umefanyika kwenye hoteli ...

Soma Zaidi