Mume auawa kwa Risasi Kibiti, mkewe ajeruhiwa kwa Risasi

Watu wasiojulikana wanadaiwa kumuua kwa kumpiga risasi, mkazi wa Kijiji cha Ruaruke, wilayani Kibiti, Mkoa wa Pwani Ramadhani Mzurui, usiku wa kuamkia leo. Kadhalika watu hao walimjeruhi mguuni kwa risasi mke wa marehemu. Mganga wa zamu katika Hospitali ya Mchukwi, Dk Emmanuel Humbi amethibitisha kufikishwa hospitalini hapo kwa mwanamke huyo akiwa na majeraha ya kupigwa risasi na kusema kwa sasa ...

Soma Zaidi

Waziri arejesha fedha za ESCROW

Aliyewahi kuwa waziri wa Nishati na Madini wakati wa Serikali ya awamu ya nne Willium Ngeleja hii leo ametangaza kuwa amezirudisha pesa za ESCROW alizopewa na mfanyabiashara James Rugemarila.

Soma Zaidi

Wenger noma, apandisha dau kumnasa mchezaji hatari toka Monaco 

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger anataka kurudi tena Monaco na dau jingine la juu baada ya madau mawili kukataliwa ili aweze kumnasa nyota Thomas Lemar, na anaamini mchezaji huyo huenda akakubali kucheza Emirates limeripoti gazeti la mirror. Kocha huyo bahili amewahi kupeleka ofa ya euro mil. 30 akachomolewa, akaongeza ikawa mil. 40 bado Monaco walimtosa na sasa anataka kufika hadi ...

Soma Zaidi

Chelsea kumsainisha star wa Madrid wakati wowote kuanzia sasa

Mabingwa wa Uingereza timu ya Chelsea iko mbioni kumsainisha nyota wa Real Madrid James Rodriguez fununu zimeeleza. Chelsea ambayo msimu inapanga zaidi kuwatumia wachezaji wake chipukizi, pia ina lengo la kuwaleta watu kama James Rodriguez, Alvaro Morata na Mateo Kovacic wote kutoka Santiago Bernabeu. Rodriguez yupo tayari kutimka klabuni hapo na inasemekana kuwa hayupo hata kwenye mpango wa kushiriki mazoezi ...

Soma Zaidi

Wyne Rooney atua Everton

Mshambuliaji wa Manchester United na mshikilizi wa rekodi ya mabao Wayne Rooney amejiunga na Everton, miaka 13 tangu aihame klabu hiyo. Rooney mwenye umri wa miaka 31 alichezea Manchester United mara 559 akifunga mabao 253. Alishinda mataji matano ya ligi kuu tangu aihame Everton kwa pauni milioni 27 mwaka 2004. “Ninahisi vizuri kurudi, sitangoja kukutana na wenzangu, kuingia mazoezini na ...

Soma Zaidi

Malinzi basi tena TFF, Warithi wake hawa hapa

Jumamosi ya July 8 2017 kamati ya uchaguzi ya shirikisho la soka Tanzania TFF ilikutana kwa mara ya kwanza baada ya kuvunjwa na kuundwa upya na kikao cha kamati ya utendaji ya TFF. Rais wa sasa wa TFF Jamal Malinzi. Baada ya kikao kumalizika na kufanya usahili wa wagombea wa nafasi zote na kuchuja, orodha ya wagombea waliyochujwa nafasi ya ...

Soma Zaidi

Mwingine auwawa kibiti

Mkazi mmoja wa kitongoji cha Nyambwanda kilichopo katika Kijiji cha Hanga wilayani Kibiti aliyetambulika kwa jina la Hamis Ndikanye (54) ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo Jumamosi akiwa nyumbani kwake. Kwa mujibu wa maelezo ya ndugu wa marehemu alijitambulisha kwa jina la Hamis Saidi amesema watu kama watano wakiwa na bunduki walifika nyumbani kwa ndugu ...

Soma Zaidi

Bodi ya mikopo Elimu yajuu yajipanga kutangaza vigezo vya wanufaika

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imesema hivi karibuni itatangaza sifa na vigezo vitakavyotumika kuwapangia wanafunzi mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2017/2018 unaotarajia kuanza miezi michache ijayo. Ufafanuzi huo umetolewa jana (Ijumaa, Julai 7, 2017) jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa HESLB, Dk Cosmas Mwaisobwa ...

Soma Zaidi