Tetesi za Soka ulaya leo

Paris Saint_Germain wana uhakika wa kukamilisha uhamisho wa pauni milioni 198 wa Neymar, 25, kutoka Barcelona katika siku 15 zijazo. (L’Equipe) Barcelona watajaribu kumsajili mshambuliaji wa Liverpool Philippe Coutinho, 25, iwapo watampoteza Neymar anayedhaniwa kuelekea PSG. (TalkSport) Philippe Coutinho ameiomba Liverpool ruhusa ya kuondoka, na tayari amefikia makubaliano ya maslahi binafsi na Barca. (RAC1) Barcelona watawapa Liverpool kiungo Ivan Rakitic ...

Soma Zaidi

Maalim Seif alia na Spika Job Ndugai, ni kuhusu ishu ya wabunge wa CUF

Katibu Mkuu wa Chama cha CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amesema kwamba hatua ya Spika kuwavua ubunge , udiwani na kuteua wengine wapya  inalenga kudhoofisha kambi ya wabunge wa  CUF na Ukawa. Amesema Watanzania wanapaswa wajikumbushe kwamba hata kama hicho kinachoitwa ‘kuwafukuza uanachama’ wabunge halali wa CUF kingekuwa kiko sawa, hatua kama hiyo hufuata taratibu zote za kisheria na kikanuni ...

Soma Zaidi

Bunge limeridhia kuvuliwa Uanachama Wabunge 8 wa CUF

Siku moja baada ya Spika wa Bunge Job Ndugai kupokea barua kutoka kwa Mwenyekiti wa CUF Taifa anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili, Prof. Ibrahim Lipumba inayoeleza kuwafukuza uanachama Wabunge wanane wa Viti Maalum na Madiwani wawili, Bunge limeridhia. Mhe. Job Ndugai. Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Leo July 26, 2017 taarifa kutoka ofisi ya Bunge imeeleza ...

Soma Zaidi

Mara Madrid, mara Man City. Mbappe aisee story ya uhamisho iko hapa

Klabu ya Monaco imeanza mazungumzo ya kumuongezea kandarasi mshambuliaji wake Kylian Mbappe kulingana na makamu wa rais wa klabu hiyo Vadim Vaslyev. Mbappe ambaye ana kandarasi hadi mwezi juni 2019 amehusishwa na uhamisho wa Real Madrid. Manchester City pia imehusishwa, lakini BBC Sport imeripoti kwamba hawako tayari kulipa kitita cha Yuro milioni 180 za uhamisho wa mchezaji huyo. Vaslyev alisema ...

Soma Zaidi

Azam yamaliza hasira kwa Lipuli

Siku mbili baada ya kufungwa 2-0 na Njombe mji, Klabu ya Azam FC, jioni hii imemaliza ziara yake huko Nyanda za Juu Kusini kwa kuichapa Lipuli FC ya Iringa mabao 4-0. Mchezo huo wa kirafiki ni sehemu ya maandalizi ya msimu ujao na ulifanyika Uwanja wa Samora mkoani humo. Azam ambayo iliweza kutawala takriban kipindi chote cha pambano hilo ilieliweza ...

Soma Zaidi

Pep Guardiola athibitisha mchezaji wake mpya ni majeruhi

Kocha Pep Guardiola amethibitisha kuwa mchezaji mpya aliyemnunua huenda asianze kutumika mwanzoni mwa msimu baada ya kugundulika ana maumivu kwenye mfupa wa paja. Nyota huyo Benjamin Mendy aliyenunuliwa kwa paundi mil. 49 akitokea Monaco, ni majeruhi na hatoweza hata kucheza pambano la kirafiki kati ya City na Real Madrid Alhamis hii. Guardiola ameweka wazi zaidi kwamba Mendy ataakaa nje kwa ...

Soma Zaidi

Mwana FA na AY Waendelea Kutamba Mahakamani

Wasanii wakongwe wa Bongo Flava, Ambwene ‘AY’ Yesaya na Hamisi ‘Mwana FA’ Mwinjuma wameendelea kupeta mahakamani wakitarajiwa kulipwa kiasi cha shilingi bilioni 2.1 na kampuni ya Mic Tanzania Limited. Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali maombi ya Kampuni hiyo ya huduma za simu za mkononi iliyotaka kukata rufaa katika Mahakama ya Rufaa kupinga amri ya kutakiwa kuwalipa ...

Soma Zaidi

Acacia “yakataa’ kuilipa serikali $ bil. 180

Serikali ya Tanzania imesema kuwa kampuni ya kuchimba dhahabu yenye makao yake nchini Uingereza Acacia inadaiwa na walipa kodi dola bilioni 180 ,kama malipo ya adhabu na riba, kulingana na taarifa ya kampuni hiyo. Lori lakubebea madini Takwimu hiyo ni kulingana na ufichuzi uliofanywa na tume mbili za rais kuhusu sekta ya uchimbaji madini. Kulingana na mwandishi wa BBC Sammy ...

Soma Zaidi

Liverpool mbioni kumnasa beki ghali kwenye historia ya soka

Klabu ya Liverpool iko katika harakati za kumnasa beki kisiki wa Southampton Virgil Van Dijk taarifa zimeeleza. Beki huyo yupo kwenye rada za kocha Klopp kwa miezi kadhaa sasa na anampango wa kuhakikisha anamjumuisha kwenye kikosi cha msimu mpya utakao anza hivi karibuni. Skysports imesema kuwa Virgil Van Dijk anayewaniwa pia na Chelsea anauzwa kwa £ mil. 60.

Soma Zaidi