YANGA INAPIGA DEILE

Mabingwa watetezi wa ligi soka ya Vodacom Tanzania Bara timu ya Yanga, wameendelea kufanya juhudi za kutaka kulinda ubingwa wao, kwa kugawa dozi kwa kila wanaye kutana nae. Timu hiyo imecheza jumanne jioni mjini shinyanga dhidi ya wenyeji wao Stand United na kufanikiwa kushinda goli 3 – 1, na hivyo inahitaji pointi nne tu ili itangaze ubingwa wa Vodacom Tanzania ...

Soma Zaidi

VIDE0: CHEKI MAGOLI MANNE KWENYE SARE YA 2-2 CHELSEA VS SPURS

Ligi kuu ya Uingereza jumatatu usiku ilikuwa na mchezo mmoja na uliwakutanisha Chelsea dhidi ya Spurs kwenye uwanja wa Stamford Bridge jijini London. Haya ndo magoli yalivyokuwa. Ndugu wasomaji wetu, mnaweza pia kupata habari zetu kwenye mitandao ya Kijamii, kwa ku Like au kutu Follow kwenye TWITER, FACEBOOK na INSTAGRAM @kwetutanzania

Soma Zaidi

LEICESTER CITY WAFALME WAPYA EPL

Timu ya Leicester City, Usiku huu imekamilisha ndoto yake ya kihistoria, iliyoingojea kwa miaka 132. Ndoto hiyo si nyingine bali ni kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza. Timu hiyo imeweza kutwaa taji hilo baada ya Tottenham kutoka sare ya 2 – 2 dhidi ya chelsea usiku huu, na hivyo kuwafanya Leicester kuwa mbele kwa point 7 ambazo haziwezi kufikiwa ...

Soma Zaidi

KIAPO CHA KUWA MJUMBE WA BARAZA LA MAWAZIRI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein leo asubuhi tarehe 02 Mei, 2016 ameapishwa kuwa mjumbe wa Baraza la Mawaziri ili aweze kushiriki na kutekeleza majukumu yake ndani ya Baraza hilo. Rais Shein ameapishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma, tukio ambalo limeshuhudiwa na ...

Soma Zaidi

JKT YAKANUSHA KUPOKEA MAOMBI YA KUJIUNGA

Jeshi la Kujenga Taifa nchini, limesema kuwa halipokei na wala halitapokea maombi yoyote ya kujiunga na mafunzo ya Jeshi hilo kwa kujitolea kwa mwaka 2016. Katika taarifa yake kwa umma inayokanusha kuhusu uvumi uliozagaa kupitia simu za mikononi na mitandao ya kijamii, unaosema kuwa “Mkuu wa jeshi JKT ametoa nafasi maalum kwa wahitimu wa taaluma ya Uandishi wa Habari wenye ...

Soma Zaidi

MAN U WAISUBIRISHA LEICESTER

Manchester United wameweza kuwazuia Leicester City kutawazwa mabingwa wa EPL jioni ya jumapili kufuatia kutoka sare ya 1 – 1 kwenye mechi iliyopigwa Old Traford. Leicester ambao walihitaji kupata pointi tatu ili kufikisha idadi ya point 79 ambazo zisingefikiwa na timu nyingine, waliweza kufungwa bao la mapema katika dakika ya 8 kufuatia kazi nzuri iliyofanywa na Anthony Martial, hata hivyo ...

Soma Zaidi

GIGGS AMWAGANA NA MKEWE

Ndoa ya mchezaji wa zamani na kocha msaidizi wa sasa wa timu ya Manchester United Ryan Giggs imeripotiwa kuvunjika baada ya mkewe kubaini Mumewe anachepuka na muhudumu wa mgahawa anaoumiliki Giggs mwenyewe. Stacey Cooke 37, ambaye ni mke wa mwanasoka huyo, ameshindwa kuvumilia kitendo hicho cha mumewe na hivyo kufungasha vilago, vyanzo imeripoti huku Giggs mwenyewe akiskika kuwaeleza watu wake ...

Soma Zaidi

YANGA YAIUA TOTO KIRUMBA

Mabingwa watetezi wa Ligi kuu ya Soka Tanzania (VPL) timu ya Yanga, imeifunga Toto Africa 2-1 katika uwanja wa CCM Kirumba siku ya jumamosi.   Katika mchezo huo, mabao yote ya Yanga yaliweza kupatikana mnamo kipindi cha pili kupitia kwa Amisi Tambwe dakika ya 50 na Juma Abdul dakika ya 78, huku bao la kufutia machozi la wenyeji Toto Africa ...

Soma Zaidi

JESHI LA POLISI LATAKIWA KUFANYA KAZI ZAKE KWA MASLAHI YA TAIFA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amelitaka Jeshi la Polisi nchini na Ofisi ya Mwendesha Mashitaka kujirekebisha kwa kutekeleza wajibu wao huku wakitanguliza maslahi ya taifa. Rais Magufuli ametoa maagizo hayo leo tarehe 29 Aprili, 2016 wakati akifungua kikao cha kazi cha Makamanda wa polisi wa mikoa, Mawakili wafawidhi wa serikali  wa Mikoa na Wakuu ...

Soma Zaidi

ALAT MPYA YAJIPANGA KUKUZA SEKTA YA VIWANDA KWENYE HALMASHAURI

Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), imetoa wito kwa Halmashauri zote nchini kutenga maeneo ya Ardhi yatakayotumika na wawekezaji kuwekeza kwenye sekta ya viwanda. Hayo yamesemwa leo jijini Dar Es Salaam na Mwenyekiti wa ALAT taifa Mhe. Diwani Gulamafeez Mukadam katika ofisi za makao makuu ya Jumuiya hiyo mbele ya waandishi wa habari, alipokuwa akianza rasmi majukumu yake ofisini ...

Soma Zaidi