Marekani kwaheri Copa America

Wenyeji wa mashindano ya Copa America Centinario 2016 timu ya soka ya taifa ya Marekani wameyaaga mashindano hayo kwa kichapo cha 4 – 0 kutoka kwa Argentina alfajiri ya leo. Marekani waliyaanza mashindano hayo ya mwaka huu mnamo juni 4 na kuchapwa bao mbili bila dhidi ya Colombia kabla kufufuka na kufanikiwa kuwashinda Costa Rica na Baadae Paraguay na kuweza ...

Soma Zaidi

KIFARU KIMEIBIWA? SIO KWELI

Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) limekanusha taarifa za kuibiwa kwa kifaru cha jeshi hilo zilizoripotiwa na gazeti la Dira na kusema kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowote, huku likisisitiza kuwa ulinzi katika maeneo ya jeshi uko imara. Akiongea na waandishi wa habari jana kukanusha habari hizo, msemaji wa jeshi hilo, Kanali Ngemela Lubinga amesema jeshi limesikitishwa sana na habari ...

Soma Zaidi

DIAMOND ANAKUJA NA P SQUARE

Rais wa WCB Wasafi Diamond Platnumz amesema kuwa mashabiki wake wakae tayari kwa ‘Hit’ kali anayotarajia kuiachia hivi karibuni akiwashirikisha wasanii wa kundi la P Square kutoka Nigeria. Ngoma hiyo ambayo mwenyewe hajafunguka lini inatoka na itaitwa jina gani, inaacha matumbo joto kwa mashabiki wake na wapenzi wa Bongo Fleva wanaomfuatilia kwa karibu wakingoja kila kona ya mitandao ya kijamii ...

Soma Zaidi

DONALD TRUMP ANUSURIKA KUUWAWA

Mwanamume mmoja raia wa Uingereza anayetuhumiwa kwa kupora bunduki ya afisa mmoja wa polisi katika mkutano wa kisaiasa wa Donald Trump, amewaambia wapelelezi wa Marekani kuwa, alitaka kumuua kwa kumpiga risasi na kumuuwa mgombea huyo wa kiti cha Urais wa chama cha Republican. Kwa mjibu wa stakabadhi za mahakama, Michael Sandford anasema kuwa aliendesha gari hadi Las Vegas akiwa na ...

Soma Zaidi

ZAIDI YA WATU 20 WAMEUWAWA LEO KWA MABOMU AFGHANISTAN

Mamlaka za Usalama nchini Afghanistan zimesema kuwa zaidi ya watu 20 wameuwa kwenye mji mkuu wa nchi hiyo Kabul katika mashambulizi tofauti ya mabomu leo jumatatu. Taarifa zaidi zinasema waliopoteza maisha ni pamoja na zaidi ya watu 14 waliokuwemo kwenye basi dogo lililokuwa limewabeba wanausalama kutoka nchini Nepal ambapo basi hilo limelipuliwa kwa bomu la kujitoa mhanga. Masaa machache baadae ...

Soma Zaidi

IGGY AZALEA NA NICK YOUNG WAMWAGANA

Rapa Iggy Azalea na mpenzi wake ambaye ni mcheza kikapu Nick Young wameachana baada ya ‘kudate’ kwa zaid ya miaka mitatu. Wawili hao wamefikia hatua hiyo baada ya muda mrefu wa kuwa kwenye malumbano yanayohusu kutokuwepo kwa uaminifu. “Ingawa nampenda Nick, na mara kadhaa nimejaribu kujenga uaminifu kwake, kwakweli katika siku za usoni nimeshindwa. Namtakia kila la kheri Nick. Haijawahi ...

Soma Zaidi

WABUNGE WA UPINZANI WAGOMA TENA LEO BUNGENI KWA STAILI MPYA

Katika kuendeleza mgomo wa kutohudhuria vikao vya Bunge litakapokuwa linaongozwa na naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson, wabunge wa upinzani mapema leo wametoka nje ya ukumbi wa Bunge hilo wakiwa wameziba midomo yao kwa mask. Mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi), James Mbatia ambaye ameongea kwa niaba ya wenzie, amesema kuwa wameamua kutumia mtindo huo mpya kwa sababu Bunge limekataa kuwasikiliza ...

Soma Zaidi

TATIZO LA MISURURU MIREFU KULIPIA TIKETI ZA MWENDOKASI LAPATA DAWA

Kampuni ya UDART inayosimamia mradi wa mabasi ya mwendo kasi, imeanzisha kadi maalum zitakazowezesha abiria kulipia nauli kwa siku saba hadi nane, na hivyo kuondoa ulazma wa kupanga msururu wa kukata tiketi kila wanapotaka kutumia usafiri huo. “kwa kuanzia tumetoa kadi 200,000 ambapo kila kadi itauzwa kwa shilingi 5000 ingawa bei halisi kwa kadi moja ni shilingi 500 na sh.4500 ...

Soma Zaidi

YANGA YAPOTEZA ALGERIA

Wawakilishi wa Tanzania kwenye mashindano ya klabu bingwa kombe la shirikisho Afrika, timu ya Yanga hapo jana jumapili imepoteza mchezo wa kwanza hatua ya makundi uliopigwa dhidi ya MO Bejaia ya Algeria kwa kufungwa bao 1 – 0. Goli hilo lililoinyima yanga pointi tatu muhimu, lilipatikana dakika ya 20 kupitia kwa mchezaji Yacine Sahli ambaye aliunganisha mpira ulioenda wavuni bila ...

Soma Zaidi

CCM KUMPA UENYEKITI JPM JULAI 23

Chama cha Mapinduzi (CCM) kinatarajia kufanya mkutano mkuu wake maalum tarehe 23 Julai mwaka huu ambapo lengo la mkutano huo likiwa ni mwenyekiti wa Sasa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kukabidhi uongozi wa huo wa chama kwa Dkt. John Pombe Magufuli. Kwa mujibu wa taarifa ya msemaji wa chama hicho Christopher Ole Sendeka, inasema Uamuzi wa kufanyika kwa mkutano mkuu huo ...

Soma Zaidi