MICHEZO

Ngao ya Jamii: Simba safari imeiva

Kikosi cha Simba kinatarajia kusafiri jioni ya leo kuelekea visiwani Zanzibar kwa ajili yakuweka kambi kujiandaa na mchezo wa ngao a hisani dhidi ya Watani wa Jadi ‘Yanga’ pamoja na maandalizi kuelekea kuanza kwa ligi kuu Tanzania Bara. 

Soma Zaidi

Nyota wa Arsenal akataa kuongeza mkataba akisubiria kusajiliwa Barca

Nyota wa Arsenal Mesut Ozil anadaiwa kuwa anakataa kusaini mkataba mpya na klabu hiyo wakati akijaribu kuskilizia dili la kuhamia Barcelona. Mchezaji huyo wa Ujerumani yupo kwenye mwaka wake wa mwisho wa mkataba wake na Gunners na atapata ongezeko la mshahara bora ikiwa ni ongezeko toka kwa mshahara wake wa sasa wa £ 140,000 chini ya mkataba wake ujao klabuni ...

Soma Zaidi

Ronaldo amuiga Messi staili ya kushangilia, mambo yakamtokea puani

Cristiano Ronaldo alitoka benchi na kuingia uwanjani, akafanikiwa kufunga bao lenye mvuto wa kipekee pale timu yake ya Real Madrid ilipoifunga Barca 3 – 1 kwenye mechi ya awamu ya kwanza ya super cup ya hispania kisha akamuiga Messi staili ya ushangiliaji. Hata hivyo, sherehe yake hiyo ilizimika muda mfupi tu, pale alipotolewa nje kwa kadi ya pili ya njano. ...

Soma Zaidi

Mkutano mkuu Simba SC: Taarifa ya kinachoendelea

Mkutano mkuu wa Wanachama wa klabu ya Simba unaendelea hivi sasa katika ukumbi wa kimataifa wa Julius Nyerere International Conference Center Mh. Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Alhaj Adam Mgoi amechaguliwa na mkutano mkuu wa Wanachama wa klabu ya Simba kuwa mdhamini wa klabu baada ya kumwondoa Mzee Kilomoni kwenye nafasi ya udhamini, pia klabu ya Simba imemsimamisha mzee Kilomoni ...

Soma Zaidi

Morocco kuwania uwenyeji wa kombe la Dunia 2026

Shirikisho la Soka la Morocco limetangaza kwamba litawasilisha ombi la kutaka kuwa mwenyekiti wa Kombe la Dunia la 2026. Uwanja wa taifa Morocco mjini Rabatt Siku ya mwisho kwa nchi kuwasilisha nia ya kuwa mwenyeji wa michuano hiyo ni leo Ijumaa, na baadaye Fifa itathibitisha nchi ambazo zimewasilisha maombi. Marekani, Canada na Mexico zilitangaza mwezi Aprili kwamba zitawasilisha ombi la ...

Soma Zaidi

‘Sub’ za Giroud na Ramsey zaiokoa Arsenal

Magoli mawili ya dakika za majeruhi yaliyofungwa na Olivier Giroud na Aaron Ramsey yameipaisha Arsenal toka kufungwa 3-2 hadi kuibuka na ushindi wa 4-3 kwenye mechi ya ufunguzi wa msimu wa ligi kuu dhidi ya Leicester City. Katika mechi ya leo, Aaron Ramsey na Olivier Giroud wameingia tokea benchi na wamefunga dakika ya 83 na 85 kwa mtiririko huo na ...

Soma Zaidi

Mkutano mkuu Simba SC: Haya hapa maamuzi ya mahakama

Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu imetupilia mbali ombi la bodi ya wadhamini wa klabu ya Simba la kutaka kuzuia mkutano Mkuu wa klabu hiyo uliopangwa kufanyika August 13 mwaka huu.  Hakimu Mkazi amesema haitokua busara kuzuia mkutano huo kwani Agenda za mkutano  hazionyeshi kama kuna agenda ya mabadiliko ya mfumo kama ambavyo wadhamini wanadai. Pia Mahakama imesema sio busara kuzuia ...

Soma Zaidi

Issue ya ‘Papaa’ Tshishimbi kuja Yanga iko hivi…

Kiungo mkabaji wa Yanga kutoka DRC Congo, Papy Kabamba Tshishimbi anatarajiwa kuwasili nchini leo Ijumaa kwa ajili ya kujiunga na timu hiyo. Tshishimbi hivi karibuni alitua nchini na kusaini mkataba wa miaka miwili ya kuichezea timu hiyo kabla ya kurejea nyumbani kwao kwa ajili ya kumaliza matatizo ya kifamilia. Awali, kiungo huyo alishindwa kujiunga na Yanga kutokana na mkataba wake ...

Soma Zaidi

Maandalizi: Simba kucheza mechi moja kisha kuiwekea kambi Yanga

Klabu ya Soka ya Simba Jumapili hii ya tarehe 13-8-2017,saa kumi alasiri itashuka kwenye Uwanja mkuu wa Taifa hapa jijini kucheza na Klabu ya Mtibwa Sugar ya Morogoro kwenye mchezo wa kirafiki.  Mchezo huo ni muhimu kwa pande zote mbili kujiandaa na Ligi kuu ya Vodacom inayotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu. Simba pia itautumia mchezo huo kuiwinda klabu ya ...

Soma Zaidi

Simba SC yaipa darasa la soka Polisi Dar

Kikosi cha Simba leo kimecheza mchezo mwingine wa kirafiki dhidi ya timu ya Polisi Dar es Salaam ambapo mpira umemalizika kwa Simba kushinda goli 2 – 1. Magoli ya Simba yamefungwa na Laudit Mavugo pamoja na Mwinyi Kazimoto.

Soma Zaidi