MICHEZO

Kylian Mbappe kukamilisha usajili kwenda PSG

Mshambuliaji wa Klabu ya Fc Monaco, Kylian Mbappe anatarajiwa kukamilisha usajili wake wa mkopo na klabu ya Ufaransa Paris Saint-Germain (PSG). Mchezaji huyo anatarajiwa kutua nchini Ufaransa siku ya Jumatatu, kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari vya Ufaransa. Kituo cha redio cha Ufaransa siku ya Jumapili kiliripoti kuwa PSG wamekubali kulipa euro milioni 180 ambazo sawa na dola ...

Soma Zaidi

Ratiba VPL yafanyiwa marekebisho 

Bodi ya Ligi (TPLB) ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limefanya mabadiliko kidogo katika michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kama ifuatavyo. Michezo ambayo imefanyiwa mabadiliko ni kati ya Tanzania Prisons na Majimaji ya Songea; Azam FC na Simba, Njombe Mji na  Young Africans; Mtibwa Sugar na Mwadui FC ambayo sasa itachezwa Septemba 6, 2017. Pia ...

Soma Zaidi

Hii hapa droo ya Champions league barani Ulaya

Draw ya klabu bingwa Ulaya 2017/18 imechezeshwa leo na pamoja mambo mengine mashabiki wa michuano hiyo watashuhudia mechi kama za Bayern v Paris, Chelsea v Atlético, Juventus v Barcelona na Real Madrid v Dortmund zikipigwa raundi hii ya kwanza. Mchezaji wa zamani wa Italia Francesco Totti akichagua jina la Chelsea ya Uingereza. Mabingwa watetezi timu ya Real Madrid ya Hispania ...

Soma Zaidi

TFF yaomba radhi makosa ya Ngao ya Jamii

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limesema kuwa linawaomba radhi wanafamilia wote wa mpira wa miguu kutokana na makosa ya maandishi yaliyoonekana kwenye utambulisho wa Ngao ya Jamii iliyotolewa Jumatano Agosti 23, 2017. Ngao hiyo ambayo ilitolewa mara baada ya mchezo uliokutanisha timu za Simba SC na Yanga SC za Dar es Salaam kwenye Uwanja Mkuu wa Taifa jijini. ...

Soma Zaidi

Tetesi za Soka ulaya leo

Baba yake Lionel Messi amezungumza na Manchester City kuhusiana na mwanae huyo kuhamia Etihad. (Sun) Barcelona wanajiandaa kupanda dau kumtaka winga wa Chelsea Willian, 29. (Times) Chelsea wamepanda dau jipya la pauni milioni 35 kumtaka winga wa Arsenal Alex Oxlade-Chamberlain, 24. (Telegraph) Chelsea wanajiandaa kutoa pauni milioni 32 kumsajili kiungo wa Leicester Danny Drinkwater, 27. (Sun) Nyota wa Chelsea Eden ...

Soma Zaidi

Simba yawasha mitambo taifa

Baada ya kutest kwa takribani miezi miwili, hii leo mnyama wa Msimbazi timu ya Simba Sc imewasha rasmi mitambo kwa kuwafunga watani wao wa jadi Young Africans Sc kwa changamoto ya mikwaju ya penati baada ya dakika 90 za kawaida kumalizika. Mashabiki wa Simva wakifurahi uwanjani. Picha ya maktaba Ilikuwa ni penati ya sita kwa upande wa Simba ambayo ilipigwa ...

Soma Zaidi

Tetesi za soka Ulaya leo

Barcelona watapanda dau la mwisho la pauni milioni 136 kumtaka kiungo wa Liverpool Philippe Coutinho, 25, baada ya dau la kwanza, la pili na la tatu kukataliwa. (Sun) Barcelona wamepanda dau la pili la pauni milioni 119  kumtaka mshambuliali wa Borussia Dortmund Ousmane Dembele, 20, lakini Dortmund wanataka pauni milioni 138. (Sky Deutschland) Barcelona wamebadili mawazo ya kumsajili kiungo wa ...

Soma Zaidi

Barcelona yamshtaki Neymar kwa kuhamia PSG

Barcelona imesema inamshtaki aliyekuwa mshambuliaji wake Neymar kwa kitita cha £7.8m kufuatia uhamisho wake katika klabu ya PSG nchini Ufaransa. Mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Brazil alivunja rekodi ya uhamisho kwa kitita cha £200m kwa timu hiyo ya Ufaransa mnamo mwezi Agosti baada ya kununua kandarasi yake katia klabu ya Barcelona . Barcelona sasa inamtaka kurudisha marupurupu aliyopewa baada ya ...

Soma Zaidi

Chirwa kuikosa Simba Ngao ya Jamii

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limemzuia kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mzambia Obrey Chirwa kucheza mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya mahasimu wao wa jadi, Simba SC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Jumatano. Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas amesema leo katika mkutano na Waandishi wa Habari mjini Dar es Salaam kwamba, Chirwa hawezi kucheza kesho kwa sababu katika ...

Soma Zaidi