MICHEZO

Matokeo yote ya mechi za VPL zilizochezwa jumamosi hii

Leo Jumamosi Mei 6, ratiba ya ligi kuu ya vodacom Tanzania bara iliendelea tena katika viwanja vitano nchini na kushuhudia mabingwa watetezi wa ligi hiyo timu ya Dar Young Africans ikirejea kileleni katika msimamo wa ligi kwa kufikisha point 59 sawa na Simba SC ikiwapiku mahasimu wao hao idadi ya mabao. Matokeo ni kama ifuatavyo Toto Africans 2 – 1 ...

Soma Zaidi

Simba kutia maguu FIFA kudai mchezaji

Klabu ya Simba imesema kuwa, itapeleka malalamiko yao katika Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kutokana na kudhulumiwa mchezaji wao, Mbaraka Yusuph anayekipiga kwenye kikosi cha Kagera Sugar. Rais wa Simba, Evans Aveva, ameyasema hayo leo mbele ya waandishi wa habari huku akiwa na leseni mkononi ya mchezaji huyo inayoonesha mwanzoni mwa msimu huu walimsajili ili aitumikie Simba, lakini wakashangaa ...

Soma Zaidi

Serengeti Boys yapangiwa Libreville

Timu ya Tanzania ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 maarufu kwa jina la Serengeti Boys, imebadilishiwa kituo kutoka Port Gentil na sasa imepangiwa Libreville. Serengeti Boys imepangwa kundi B pamoja na timu za Niger, Angola na Mali ambako watafungua nayo mchezo Mei 15, mwaka huu. Kwa mabadiliko hayo, Kundi A lenye timu za Cameroon, Ghana, Guinea pamoja ...

Soma Zaidi

Fainali za AZAM Sports Federation Cup kupigwa Dodoma

Mchezo wa Fainali za kuwania Kombe la Shirikisho la Azam (Azam Sports Federation Cup HD – ASFC), kati ya Simba SC ya Dar es Salaam na Mbao FC ya Mwanza, utafanyika Mei 28, mwaka huu kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma. Kwa mujibu wa Kanuni ya 5 ya michuano ya ASFC kuhusu Uwanja wa mashindano inasema: “Uwanja wa mashindano ya ...

Soma Zaidi

Yanga yazungumzia ishu yake ya kutema wachezaji inayojadiliwa mitandaoni

Katibu mkuu Yanga SC anapenda kutoa taarifa kwa vyombo vya habari na wadau wa soka nchini kuhusiana na taarifa mbalimbali zinazoendelea katika mitandao ya kijamii na vituo vya redio kuhusu klabu hii kuwa na mpango wa kuwaacha baadhi ya wachezaji. Taarifa hizo ni za uongo na uzushi mkubwa . Uongozi upo bega kwa bega na wachezaji wote 27 na benchi ...

Soma Zaidi

Haji Manara apigwa pini

Kamati ya Nidhamu ya TFF, imemuhukumu kifungo cha miezi 12 kujihusisha na soka ndani na nje ya nchi na jumla ya fainali ya Sh milioni tisa baada ya kumtia hatiani kwa makosa ya kukashifu, kutuhumu, kudhalilisha, kupotosha na kushawishi kupata ushindi wakati kuna shitaka lipo kwenye kamati.

Soma Zaidi

Hiki hapa kikosi cha Yanga SC dhidi ya Prisons kombe la shirikisho

​Mchezo wa mwisho wa robo fainali ya kombe la shirikisho (ASFC) unatarajiwa kupigwa leo katika uwanja wa taifa ambapo utawakutanisha Mabingwa wa tetezi wa kombe hilo dhidi ya Tanzania Prisons toka mkoani Mbeya. Hii hapa ni line up ya kikosi cha Yanga. 1. Beno Kakolanya 2. Hassani Kessy 3. Haji Mwinyi 4. Kelvin Yondani 5. Nadir Haroub 6. Juma Makapu ...

Soma Zaidi

Haji Manara aitwa kikaangoni TFF

Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania (TFF) limempeleka mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa mabingwa wa zamani wa Tanzania Simba SC Bw. Haji Manara kwenye Kamati ya nidhamu ili kwenda kusomewa mashtaka yanayomkabili. Taarifa iliyotolewa na shirikisho leo Ijumaa inasemeka kuwa, kwa mujibu wa Katiba ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kila mwanafamilia wa mpira ...

Soma Zaidi

Ilichokisema Simba kuhusu marejeo ya rufaa yao iliyowapa point tatu

​Uongozi wa klabu ya Simba umesema hakukuwa na haja ya Kamati ya Katiba Sheria na Hadhi za wachezaji kuitisha kikao kwa ajili ya kujadili marejeo (Review) ya shauri la timu ya Kagera Sugar kwa madai kuwa haina uhalali huo. Kauli hiyo inakuja siku moja baada ya Kamati hiyo kukutana jana kwenye Hotel ya Protea kupitia shauri hilo ambapo mpaka sasa ...

Soma Zaidi