HABARI

Breaking News! Soko la SIDO mbeya linateketea

Taarifa zilizotufikia usiku huu kutoka mkoani Mbeya, zinaeleza kuwa soko la Sido lililopo Mwanjelwa jijini humo linateketea kwa moto. Hadi sasa chanzo cha moto huo hakijafaahamika lakini inaelezwa maduka kadhaa yameungua yakiwa na mali zenye thamani kubwa. Tutaendelea kukujuza juhudi za kuudhibiti zimefikia wapi.

Soma Zaidi

Lipumba Amwangukia Maalim Seifu… Amtaka Arudi Ofisini, Wakutane na Kumaliza Tofauti zao

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) anayetambuliwa na msajili wa Vyama Vya Siasa nchini Profesa Ibrahim Lipumba amemtaka Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad kurudi wafanye mazungumzo na kumaliza tofauti. Profesa Lipumba amesema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Makao Makuu ya ofisi za Chama Cha Wananchi (CUF) zilizopo Buguruni. Lipumba amemtaka Katibu Mkuu ...

Soma Zaidi

Yaliyojiri kwenye ziara ya Rais wa Misri nchini

Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri Mhe. Abdel Fattah El-Sisi leo tarehe 15 Agosti, 2017 amemaliza ziara yake rasmi ya kiserikali ya siku mbili aliyoifanya hapa nchini kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam Mhe. Rais El-Sisi ameagwa ...

Soma Zaidi

China yapiga marufuku bidhaa za Korea Kaskazini

China imesema itasitisha mpango wa kununua makaa ya mawe, chuma na chakula cha baharini kutoka Korea Kaskazini. Hatua hiyo ni ya utekelezaji wa vikwazo vya Umoja wa Mataifa vilivyowekwa kutokana na hatua ya Korea kaskazini kufanyia majaribio makombora yake mawili ya masafa marefu mwezi uliopita. China inanunua asilimia 90 ya biashara yote ya Korea kaskazini. Beijing ilikuwa imeahidi kuweka vikwazo ...

Soma Zaidi