HABARI

LHRC Waungana na TLS Kupinga Ofisi za Mawakili Kupigwa Bomu

Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika ‘TLS’, ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ameendelea kulaani tukio la kuvamiwa ofisi za Wanasheria IMMMA Advocates na kusema ni muhimu jambo hilo likapigiwa kelele kwa kuwa siyo la kisiasa. Lisu amesema hayo baada ya kualikwa katika mkutano wa kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)na kusema kuna mashirika mengi ...

Soma Zaidi

Yaliyojiri Ikulu leo Agosti 24, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 24 Agosti, 2017 amemuapisha Brigedia Jenerali John Julius Mbungo kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU). Hafla ya kuapishwa kwa Brigedia Jenerali John Julius Mbungo imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu ...

Soma Zaidi

Dereva Aliyegonga Treni Morogoro na Kuua Watatu Atiwa Mbaroni

Jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro linamshikilia dereva wa basi lenye namba za usajili T 438 ADR Charles Diamond, kwa kusababisha ajali iliyopoteza uhai wa watu mkoani Morogoro na kusababisha majeraha kwa baadhi ya watu. Akitoa taarifa ya ajali hiyo iliyotokea leo asubuhi Kamanda wa Polisi mkoani humo Urlich Matei, amesema mpaka sasa idadi kamili ya watu waliofariki kutokana na ...

Soma Zaidi

Magazeti yote Tanzania yanatakiwa kusajiliwa upya

Msemaji wa Serikali Dk Hassan Abbasi amesema kwamba kuanzia leo hadi Oktoba 15, Magazeti yote yataanza kusajiliwa upya. “Baada ya Oktoba 15, 2017 hakuna atakayeruhusiwa kuchapisha bila usajili”Amesema Dk Abbasi na kuongeza; “Mfumo mpya wa utoaji wa leseni kwa machapisho yote umeanza rasmi leo ‘’ Amesema taratibu zote za upatikanaji wa leseni zimewekwa katika tovuti http://www.maelezo.go.tz “- Mawasiliano kwa ajili ...

Soma Zaidi

Serikali Kununua Rada 4 za Kisasa

Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Anga (TCAA) jana (Jumanne) imeingia makubaliano na kampuni inayojihusisha na mifumo ya anga kutoka nchini Ufaransa ya Thales kununua rada mpya nne. Tukio hilo lilishuhudiwa na Waziri wa Ujenzi uchukuzi na mawasiliano Profesa Makame Mbarawa na wadau wengine wa usafiri wa anga nchini. Upande wa Serikali mkataba ulisainiwa na Mkurugenzi wa Mkuu wa TCAA ...

Soma Zaidi

Wanne washtakiwa kwa kula nyama za watu

Wanaume wanne wamefikishwa kwenye mahakama ya Afrika Kusini kujibu mashtaka ya ulaji nyama ya binadamu, baada ya madai kuwa mmoja wao alifika katika kituo cha polisi na kusema kuwa amechoka kula nyama ya binadamu. Alipohojiwa zaidi mwanamume huyo alionyesha sehemu ya mguu na mkono wa binadamu. Kisha polisi wakaandamana na mwanamume huyo hadi kwa nyumba moja iliyo mtaa wa KwaZulu-Natal, ...

Soma Zaidi