HABARI

TPA yakamata makontena mengine 262 yenye mchanga wa madini Bandari kavu Dar

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imebaini makontena mengine 262 yenye mchanga wa dhahabu yaliyokuwa yamehifadhiwa katika bandari kavu ya MOFED (zamani ZAMCARGO) iliyopo Kurasini jijini Dar es salaam yakisubiri taratibu za kiforodha kabla ya kusafirishwa kwenda nje ya nchi kupitia kitengo cha makontena kinachoendeshwa na kampuni binfasi ya TICTS. Kubainika kwa makontena hayo kumekuja siku tatu tu baada ...

Soma Zaidi

Nani kasema Kinana anaongea na waandishi leo?

​Kumekuwepo na taarifa  mitandaoni zikisema kuwa katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Abdulrahman Kinana ameitisha mkutano na waandishi wa habari. Taarifa hizo zimekanushwa na katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho Humphrey Polepole, ambaye katika ukurasa wake wa twitter, Polepole amesema “Napenda kukanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni kwamba Katibu Mkuu wa CCM Komrade Kinana atakuwa na Mkutano na ...

Soma Zaidi

Mwigulu Nchemba ashangazwa na polisi kumtolea Nape Bastola, atoa agizo kwa IGP

​Aliyekuwa waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye jana alizuiliwa kufanya mkutano na waandishi wa habari katika hoteli ya Protea jijini Dar ambapo askari kanzu mmoja alifikia kutoka bastola ili kumshinikiza kiongozi huyo arudi kwenye gari.  Sasa Mhe. Mwigulu Nchemba ambaye ni waziri wa Mambo ya ndani ya nchi leo kwenye ukurasa wake wa twitter amesema haya ...

Soma Zaidi

JPM afanya ziara ya kushtukiza Bandarini kufuatilia maelekezo aliyotoa

​Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 23 Machi, 2017 amefanya ziara ya kushtukiza katika bandari ya Dar es Salaam kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa maelekezo aliyoyatoa kwa nyakati tofauti juu ya kudhibiti udanganyifu wa mizigo inayoingia na kutoka nchini kupitia bandari hiyo ikiwemo usafirishaji wa mchanga wa madini kwenda nje ya ...

Soma Zaidi

Breaking Newzzz! Magufuli amtema Nape uwaziri

​Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 23 Machi, 2017 amefanya mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri. Katika Mabadiliko hayo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Prof. Palamagamba Aidan John Mwaluko Kabudi kuwa Waziri wa Katiba na Sheria. Aidha, Mhe. Dkt. Magufuli amemteua Dkt. Harrison George Mwakyembe kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. ...

Soma Zaidi

Polisi: shambulio la London ni la kigaidi

Polisi jijini London wamesema shambulio la siku ya Jumatano katika daraja la Westminster na nje ya bunge la nchi hiyo yanaweza kuhusishwa na itikadi kali ya kiislamu. Polisi mwandamizi kuhusu masuala ya ugaidi, Mark Rowley, pia amesema wanaamini wanaweza kumtambulia mshambuliaji wa tukio hilo, lakini hakutoa taarifa zaidi. Raia watano wameuawa na wengine zaidi ya arobaini kujeruhiwa na mtu aliyevurumiza ...

Soma Zaidi

Madaktari Kenya Wawaonya Madaktari wa Tanzania Wanaotaka Kwenda Kenya

Chama cha Madaktari wa Kenya (KMPDU), kimewataka wenzao wa Tanzania wasikubali kusaini mkataba wowote wa kwenda Kenya kabla mgogoro wao na Serikali haujatatuliwa. Taarifa ya KMPDU  inasema haina tatizo na uwezo ama mafunzo ya madaktari wa Tanzania na protokali ya leseni za madaktari inayotambulika na Baraza na Bodi za nchi za Afrika Mashariki. “Lakini tunapenda kuwataarifu kwamba kwa miaka miwili ...

Soma Zaidi

TEF yamtangaza Makonda adui wa uhuru wa habari

Jukwaa la Wahariri Tanzania(TEF) leo  limevitaka vyombo vya habari nchini kutokuandika au kutangaza habari zozote zinazomhusisha Mkuu wa Mkoa wa  Dar es Salaam, Paul Makonda. TEF wameyasema hayo leo katika  taarifa yao na kulaani vikali kitendo cha Makonda cha kuvamia kituo cha Utangazaji cha Clouds usiku wa Machi 17 akiwa na askari wenye silaha. “Kwa mantiki hiyo, tunamtangaza Ndugu Paul ...

Soma Zaidi

Forbes: Mabilionea 25 matajiri zaidi Afrika 2017

Mfanyabiashara kutoka Nigeria Aliko Dangote bado ndiye mtu tajiri zaidi barani Afrika kwa mujibu wa orodha ya mabilionea mwaka 2017 iliyoandaliwa na jarida la Forbes. Utajiri wa Dangote unakadiriwa kuwa jumla ya $12.2 bilioni. Kuna mabilionea (wa Dola) 25 mwaka huu barani Afrika, mmoja juu ya 24 waliokuwepo mwaka jana. Wafanyabiasha kutoka Nigeria Femi Otedola na Abdulsamad Rabiu hawakufanikiwa kuingia ...

Soma Zaidi