HABARI

Tundu Lissu apigwa risasi na watu wasiojulikana Dodoma

Taarifa zilizotufikia zinasema Mbunge wa Singida Mashariki, ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu amepigwa risasi akiwa Dodoma. Tairi la mbele la gari linalodaiwa kuwa la Tundu Lissu na alama zinazodaiwa kuwa za risasi zilizopigwa kwenye kioo, kama  zinavyoonekana. Aidha mbunge huyo amekimbizwa kwenye hospitali kuu ya mkoa kwa ajili ya huduma ya kwanza na matibabu. Tutaendelea kukujuza kinachoendelea. ...

Soma Zaidi

Kijana wa Miaka 18 Asimulia Jinsi Alivyowateka Watoto Wanne Arusha

Matukio ya utekaji watoto mjini Arusha yameanza kupata mwelekeo wa ufumbuzi baada ya kijana wa miaka 18 kukiri kuwateka watoto wanne alipokamatwa katika mji wa Katoro wilayani Geita alikofanya tukio jingine la utekaji. Akizungumza mbele ya waandishi wa habari akiwa chini ya ulinzi wa polisi jana, kijana huyo aliyejitambulisha kwa jina la Samson Petro alisema watoto wawili aliwarudisha kwa wazazi ...

Soma Zaidi

Njiwa atumika kuingiza dawa za kulevya Gerezani

Polisi nchini Argentina walimpiga risasi njiwa ambaye alitumiwa kusafirisha mihadarati kwenda gereza moja, kwa mujibu wa mamlaka za gereza. Njiwa huyo alionekana akiruka hadi uwanja wa gereza lililo mji wa Santa Rosa. Maafisa waligundua kuwa ndege huyo alikuwa amefungiwa mfuko mdogo kwenye mgongo wake uliokuwa na tembe za madawa ya kulevya. Njia hiyo ya kusafirisha madawa ilikuwa imegunduliwa na ilikuwa ...

Soma Zaidi

Baraza la usalama la UN laionya Korea Kaskazini

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limelaani kitendo cha Korea Kaskazini cha kurusha kombora kupitia anga ya Japan, huku nchi hiyo ikithibitisha kutekeleza. Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong-un Taarifa iliyoandikwa na Marekani, haikutishia kuiwekea vikwazo vipya Korea kaskazini. Lakini Baraza la Usalama limeitaka Korea Kaskazini kusitisha majaribio zaidi na kusitisha mpango wake wa nuklia. Wanachama 15 wa Baraza ...

Soma Zaidi

Kim Jong-un: Tutarusha makombora zaidi Pacific

Kombora lililorushwa siku ya Jumanne lilipitia juu ya kisiwa cha Japan cha Hokaido na kusababisha hali ya wasiwasi wa kusalama huku raia wakitakiwa kujificha kabla ya kombora hilo kuanguka baharini. Vyombo vya habari vya taifa hilo pia vilirejelea vitisho katika kisiwa cha Marekani cha Guam katika bahari ya Pacific ambacho imesema inamiliki kambi ya uvamizi wa kijeshi wa Marekani. Baraza ...

Soma Zaidi