HABARI

Bajeti mpya, Road License yafutwa na sasa kulipwa mara moja

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango ametangaza kufutwa rasmi kwa ada ya mwaka ya leseni ya magari. Amesema uamuzi umechukuliwa ili ada hii ilipwe mara moja pale gari linaposajiliwa na baada ya hapo iendelee kulipwa katika ushuru wa bidhaa katika mafuta ya petroli na dizeli. Hayo yameelezwa leo Alhamisi bungeni na Waziri Mpango wakati akiwasilisha bajeti ya mwaka ...

Soma Zaidi

Mmoja apigwa risasi Rufiji, na wawili waokotwa wakiwa wamekufa

Nurdin Mohammed Kisinga ,amejeruhiwa baada ya kupigwa risasi ya kichwa ,na watu wasiojulikana huko kijiji cha Ngomboroni kata ya Umwe Kaskazini, Ikwiriri wilayani Rufiji. Katika hatua nyingine watu wawili wenye jinsia ya kiume,wameokotwa wakiwa wamefariki dunia wilayani Rufiji na mwingine Kibiti. Akielezea tukio la kupigwa risasi ,mkuu wa wilaya ya Rufiji, Juma Njwayo,alisema limetokea saa saba mchana, june 7 wakati ...

Soma Zaidi

JWTZ yatoa ONYO kwa matapeli wa ajira

Mkuu wa utumishi Jeshi la Wananchi Tanazania (JWTZ), Meja Jenerali  Harrison Masebo amekanusha taarifa  zinazoenea mitandaoni kuhusu kutangazwa kwa nafasi za ajira na kwamba watu wanaotangaza hivyo ni matapeli waepukwe. Meja Jenerali Masebo amebainisha hayo baada ya kuenea uvumi mitandaoni na mitaani kwa baadhi ya watu kujifanya wanahusika na jeshi hilo katika idara ya kutoa ajira kwa wananchi. “Kumekuwa na ...

Soma Zaidi

Mwanasheria mkuu wa TBS afikishwa Mahakamani

Mwanasheria Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Baptister Marco (54) amepandishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka matatu ya kuishi na kufanya kazi nchini bila kuwa na  kibali. Mwendesha Mashtaka wa Uhamiaji, Novatus Mlay alimemsomea mashtaka hayo leo Jumatano kwa Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa. Akisoma hati ya mashtaka,  Mlay alidai kuwa  Mei 19, 2017  huko Kinondoni katika ...

Soma Zaidi

JPM amuapisha rasmi mama Anna Mghwira

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 06 Juni, 2017 amemuapisha Bibi Anna Elisha Mghwira kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro. Bibi Anna Elisha Mghwira amejaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Saidi Meck Sadiki aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo. Hafla ya kuapishwa kwa Bibi Anna Elisha Mghwira imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam ...

Soma Zaidi