HABARI

Korea Kaskazini: Hotuba ya Trump ni sawa na mbwa anayebweka

Mwanadiplomasia wa cheo cha juu wa Korea Kaskazini ameifananisha hotuba ya Trump kwa Umoja wa Mataia na kibweko cha mbwa. Akihutubia baraza kuu la Umoja wa Mataifa siku ya Jumatano, Bw Trumo alisema kuwa ataiharibu Korea Kaskazini ikiwa itakuwa tisho kwa Marekani na washirika wake. Matamshi ya waziri wa mashauri ya nchi za kigeni Ri Yong-ho, ndiyo ya kwanza rasmi ...

Soma Zaidi

Serikali yaendelea kuzuia almasi ya kampuni ya Petra

Shughuli zimeanza tena katika mgodi mkubwa zaidi wa madini ya almasi nchini Tanzania, licha ya mzozo na serikali ya Tanzania, ambayo ilikamata bahasha iliyokuwa na almasi kwenye uwanja wa ndege. Shughuli katika mgodi wa Williamson zimerejeshwa baada ya kusimamishwa kwa siku nne. Wiki moja iliyopita hisa kwenye kampuni ya Uingereza ya Petra zilishuka kwa asilimia 7, baada ya almasi zake ...

Soma Zaidi

‘Waziri’ Ngeleja ahojiwa na ofisi ya DCI

Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja amehojiwa kwa saa moja katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Septemba 11. Ngeleja ambaye pia amewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini wa awamu ya nne, aliwasili katika ofisi hiyo saa nne asubuhi akiwa peke yake ambapo alikutana na DCI saa tano na kuondoka saa sita ...

Soma Zaidi

Magufuli atoa kauli hii, kuhusu yeye kusaini wafungwa wanaotakiwa kunyongwa

Rais John Pombe Magufuli amefunguka na kutoa kauli yake kuhusu baadhi ya wafungwa ambao wamehukumiwa kunyongwa kutokana na makosa mbalimbali na kudai kuwa yeye anaogopa kusaini ili wafungwa hao wanyongwe. Rais Magufuli amesema hayo leo Ikulu jijini Dar es Salaama wakati akimuapisha Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma na kusema anatambua kuwa idadi wa wafungwa waliohukumiwa kunyongwa ni ...

Soma Zaidi

Huu ndio waraka alioutoa Mhe. Mbowe juu ya swala zima la Lissu kupigwa Risasi na hali yake ilivyo sasa

Kufuatilia shambulio la kikatili la risasi alilofanyiwa Mhe. Tundu Lissu na dereva wake,  Simon   Mohammed Bakari siku ya Alhamisi, 7 Septemba 2017, mjini Dodoma na kuhamishiwa katika JIji la Nairobi siku hiyo hiyo usiku kwa ajili ya matibabu na usalama, napenda kutoa taarifa zifuatazo kwa Watanzania wote. Mhe. Tundu Lissu UAMUZI WA KUMLETA NAIROBI BADALA YA DAR ES SALAAM. Tulilazimika ...

Soma Zaidi