kwetutanzania Newsroom

Vikosi vya mechi ya Azam FC vs Simba SC chamazi

Mpambano wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara ambao uliokuwa ukisubiriwa na wengi, ni kati ya Azam FC vs Simba SC unatarajiwa kuanza dakika chache zijazo kutoka kati kiwanja cha Azam Complex kule Chamazi jijini Dar.  Tizama vikosi hapa AZAM FC SIMBA SC 1. Aishi Manula 2.Ally Shomari 3.Erasto Nyoni 4.Salim Mbonde 5.Method Mwanjale 6.James Kotei 7.Haruma Niyonzima 8.Mzamiru Yassin ...

Soma Zaidi

Costa kutimkia Fenerbahce?

Klabu ya Fenerbahce ya Uturuki imefanya mazungumzo na wawakilishi wa mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa kuhusu uwezekano wa kumchukua kwa mkopo. Costa, 28, amesalia nchini Brazil na amekataa kurejea England. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania alishindwa kuhama kutoka kwa mabingwa hao wa Ligi ya Premia kabla ya siku ya mwisho ya kuhama wachezaji katika ligi nyingi kuu Ulaya. Hata ...

Soma Zaidi

Kutoka Bungeni: Huu ndio undani wa Tukio zima la Mhe. Lissu kupigwa risasi jana.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai, ametoa taarifa ya kina kuhusu tukio zima la kupigwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA Mh. Tundu Antiphas Lissu. Bunge limetoa taarifa kupitia akaunti yake rasmi ya mtandao wa twitter, huku likisema kuwa Mhe. Lissu alipigwa jumla ya risasi tano na watu wasiojulikana kisha ...

Soma Zaidi

Alichokisema JPM kuhusu tukio la Tundu Lissu kupigwa Risasi

Kufuatia tukio la Mbunge wa Singida Mashariki, ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu kupigwa risasi mchana wa leo ambapo alijeruhiwa vibaya sehemu mbalimbali katika mwili wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  ametuma salamu za pole. Mhe. Tundu Lissu Kupitia akaunti yake ya mtandao wa twitter, Rais Magufuli ameelezea mstuko alioupata ...

Soma Zaidi

Hii hapa ratiba yote ya VPL wikendi hii

Mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara unatarajiwa kuendelea tena mwishoni mwa wiki hii, ambapo siku ya Jumamosi kutakuwa na michezo miwili na Jumapili Septemba 10 kutakuwa na michezo sita. Ligi hiyo ilisimama ili kupisha mechi za kimataifa za kufuzu kucheza kombe la Dunia mwakani nchini Urusi, na kwa zile timu zisizogombea kushiriki kombe hilo, zilicheza michezo ...

Soma Zaidi

Tundu Lissu apigwa risasi na watu wasiojulikana Dodoma

Taarifa zilizotufikia zinasema Mbunge wa Singida Mashariki, ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu amepigwa risasi akiwa Dodoma. Tairi la mbele la gari linalodaiwa kuwa la Tundu Lissu na alama zinazodaiwa kuwa za risasi zilizopigwa kwenye kioo, kama  zinavyoonekana. Aidha mbunge huyo amekimbizwa kwenye hospitali kuu ya mkoa kwa ajili ya huduma ya kwanza na matibabu. Tutaendelea kukujuza kinachoendelea. ...

Soma Zaidi

Kijana wa Miaka 18 Asimulia Jinsi Alivyowateka Watoto Wanne Arusha

Matukio ya utekaji watoto mjini Arusha yameanza kupata mwelekeo wa ufumbuzi baada ya kijana wa miaka 18 kukiri kuwateka watoto wanne alipokamatwa katika mji wa Katoro wilayani Geita alikofanya tukio jingine la utekaji. Akizungumza mbele ya waandishi wa habari akiwa chini ya ulinzi wa polisi jana, kijana huyo aliyejitambulisha kwa jina la Samson Petro alisema watoto wawili aliwarudisha kwa wazazi ...

Soma Zaidi

Njiwa atumika kuingiza dawa za kulevya Gerezani

Polisi nchini Argentina walimpiga risasi njiwa ambaye alitumiwa kusafirisha mihadarati kwenda gereza moja, kwa mujibu wa mamlaka za gereza. Njiwa huyo alionekana akiruka hadi uwanja wa gereza lililo mji wa Santa Rosa. Maafisa waligundua kuwa ndege huyo alikuwa amefungiwa mfuko mdogo kwenye mgongo wake uliokuwa na tembe za madawa ya kulevya. Njia hiyo ya kusafirisha madawa ilikuwa imegunduliwa na ilikuwa ...

Soma Zaidi