kwetutanzania Newsroom

Droo ya UEFA 16 Bora, huku Ronaldo kule Neymar

Mabingwa watetezi Real Madrid watakutana na Paris Saint-Germain katika mechi za mzunguuko wa mzunguuko wa 16 bora  ya Ligi ya Mabingwa wakati Chelsea itakuwa na kibarua dhidi ya Barcelona. Manchester United imepangwa dhidi ya Sevilla, Manchester City kucheza na Basel huku Liverpool ni dhidi ya Porto nchini Ureno wakati Tottenham Hotspur wana mtihani mgumu wa kumenyana na vijana kutoka Torino ...

Soma Zaidi

Guardiola aitangaza siku ya kubeba ubingwa 

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola ametabiri timu yake itanyakua taji la Ligi Kuu ifikapo Aprili mwakani ikiwa wimbi la ushindi la sasa litaendelea. Jana City iliwapiga mahasimu wao Manchester United 2-1 katika awamu ya kwanza ya Manchester derby kwenye dimba la Old Trafford na sasa wako mbele kwa tofauti ya point 11 kwenye msimamo wa ligi huku Guardiola akitamba ...

Soma Zaidi

Korea Kaskazini: Hotuba ya Trump ni sawa na mbwa anayebweka

Mwanadiplomasia wa cheo cha juu wa Korea Kaskazini ameifananisha hotuba ya Trump kwa Umoja wa Mataia na kibweko cha mbwa. Akihutubia baraza kuu la Umoja wa Mataifa siku ya Jumatano, Bw Trumo alisema kuwa ataiharibu Korea Kaskazini ikiwa itakuwa tisho kwa Marekani na washirika wake. Matamshi ya waziri wa mashauri ya nchi za kigeni Ri Yong-ho, ndiyo ya kwanza rasmi ...

Soma Zaidi

Mahakama yamfungia Rooney miaka miawili

Nahodha wa zamani wa kikosi cha England Wayne Rooney amefika mahakamani na kukiri kuendesha gari akiwa mlevi. Alikamatwa wakati polisi walisimamisha gari lake huko Wilmslow, Cheshire tarehe mosi mwezi Septemba. Rooney 31 alipigwa marufuku ya kuendesha gari kwa miaka miwili na kuamrishwa kutoa huduma ya jamii bila malipo kwa masaa 100. Rooney pia aliamrishwa kulipa pauni 170 wakati alifika katika ...

Soma Zaidi

Serikali yaendelea kuzuia almasi ya kampuni ya Petra

Shughuli zimeanza tena katika mgodi mkubwa zaidi wa madini ya almasi nchini Tanzania, licha ya mzozo na serikali ya Tanzania, ambayo ilikamata bahasha iliyokuwa na almasi kwenye uwanja wa ndege. Shughuli katika mgodi wa Williamson zimerejeshwa baada ya kusimamishwa kwa siku nne. Wiki moja iliyopita hisa kwenye kampuni ya Uingereza ya Petra zilishuka kwa asilimia 7, baada ya almasi zake ...

Soma Zaidi

Kocha huyu awa wa kwanza kujiuzuru VPL msimu huu

Uongozi wa Njombe mji FC unapenda kuwaarifu wanafamilia wa soka kuwa Kocha mkuu wao ameandika barua ya kuacha kuifundisha timu hiyo. Kocha huyo ndugu Ahmed Hassan Banyai ameachia ngazi kwa hiari yake siku ya Jumatatu, na barua amekwisha ikabidhi kwa uongozi. Wakati huohuo kocha msaidizi ndudu Mrage Kabange atasimamia timu kwa sasa mpaka hapo uongozi utakavyoamua nani awe kocha mkuu. ...

Soma Zaidi