Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 11.09.2017

Meneja wa zamani wa timu ya taifa ya England Roy Hodgson anapigiwa upatu kuchukua nafasi ya Frank de Boer ambaye amefutwa kazi Crystal Palace baada ya kuwaongoza kwa mechi nne pekee. (Daily Mirror)

Antoine Griezmann alihamia Atletico Madrid kutoka Real Sociedad mwaka 2014

Sam Allardyce pia anahusishwa na kazi hiyo ya Palace. (Daily Mail)

Manchester United wamehifadhi jezi nambari saba kwa ajili ya mshambuliaji Antoine Griezmann, 26, ambaye wanaamini wanaweza mwishowe kufanikiwa kumchukua kutoka Atletico Madrid kwa £100m. (Daily Star)

Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa ameihamishia familia yake Madrid akiendelea kutarajia kwamba maafikiano yatapatikana kumuwezesha kurejea Atletico. (Football 365)

Chelsea wako tayari kushindana na Barcelona kumnunua kiungo wa kati chipukizi anayethaminiwa sana Bayer Leverkusen Atakan Akkaynak, 18. (Daily Express)

West Ham wamemchagua kocha wa Napoli Maurizio Sarri kama mtu ambaye wanataka ajaze nafasi ya meneja Slaven Bilic. (Daily Express)

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger anaamini uamuzi wa Neymar wa kuondoka Barcelona kwenda Paris St-Germain uliongozwa na pesa na si ndoto kuu anayotaka kuitimiza. Wenger amesema uamuzi huo unaonesha mchezaji huyo wa miaka 25 hataki kucheza na wachezaji bora zaidi. (BeIn Sports – kupitia Goal.com)

Shughuli za Arsenal katika soko la kuhama wachezaji zinaweza kubadilika kwani mtu anayeongoza kuwatafuta wachezaji – Dick Law – anatarajiwa kuacha majukumu hayo, lakini Arsene Wenger amekanusha kwamba afisa mkuu mtendaji Ivan Gazidis atachukua majukumu ya Law. (Evening Standard)

Wenger amefichua kwamba ni “maadili” katika Arsenal ambayo yalimshawishi kukataa kwenda Manchester United walipomuomba ahamie huko kujaza nafasi ya Sir Alex Ferguson kama meneja Old Trafford alipostaafu. (Independent)

Afisa mkuu mtendaji Manchester United Ed Woodward atatumia ufanisi wa klabu hiyo kibiashara kuwavutia Gareth Bale, 28, wa Real Madrid na Antoine Griezmann, 26, wa Atletico Madrid katika klabu hiyo majira yajayo ya joto. (Manchester Evening News)

Mkufunzi mkuu wa Stoke City Mark Hughes huenda akatozwa faini kwa kumsukuma Jose Mourinho kwenye eneo la wakufunzi uwanjani wakati wa sare yao na Manchester United Jumamosi. (The Times)

Nyota wa zamani wa Bayern Munich Stefan Effenberg anaamini mabingwa hao wa Ujerumani wanafaa kufikiria uwezekano wa kumuuza Robert Lewandowski baada ya mshambuliaji huyo “kukosoa filosofia” ya klabu hiyo kwenye vyombo vya habari. (t-online.de – kupitia Goal.com)

Mdosi wa Manchester City Pep Guardiola anamtaka mchezaji wa Tottenham Toby Alderweireld, 28, awe mrithi wa muda mrefu wa Vincent Kompany safu ya ulinzi ya kati. (Football 365)

Guardiola amekerwa na Kompany baada ya mchezaji huyo kucheza dakika 90 kwenye timu ya taifa licha ya kuumia kwenye misuli ya chini ya mguu. (Daily Mirror)

Mchezaji wa Liverpool Danny Ings anaonekana kupata pigo jingine katika kujaribu kupata nafuu kutokana na jeraha baada ya kushindwa kumaliza dakika 90 akiwa na timu ya vijana wa chini ya miaka 23 katika klabu hiyo.

Straika huyo wa miaka 25 ametatizwa na majeraha ya goti kwa misimu miwili iliyopita. (The Sun)

Kocha wa zamani wa Barcelona Luis Enrique alikuwa amepanga kupumzika kwa msimu mmoja lakini huenda akarejea kazini Januari katika klabu ya Shanghai Shenhua ya China baada ya klabu hiyo kuwasiliana naye kuhusu uwezekano wake kuchukua nafasi ya Gustavo Poyet. (TMW – kupitia Marca)

Carlo Ancelotti huenda akaihama Bayern Munich kufikia Januari, kwa mujibu wa mchezaji wa zamani Mario Basler, anayesema Mwitaliano huyo ametia saini mkataba wa kuhamia klabu moja China. (Sport1 – kupitia Daily Mail)

Mkufunzi wa Brighton Chris Hughton amesema klabu hiyo inahitaji kumnunua mshambuliaji mwingine. (Daily Mail)

BBC

Comments

comments