Manchester City 5 – 0 Liverpool, Sadio mane apigwa umeme

Manchester City imetumia fursa ya kutolewa kwa kadi nyekundu Sadio Mane na kuweza kuitungua Liverpool 5-0 katika mpambano wa kusisimua kwenye Ligi Kuu ya Uingereza Uwanja wa Etihad.

Mane alioneshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja katika nusu ya kwanza ya mechi hiyo kwa kumfanyia rafu mbaya Ederson ambayo imesababisha kipa wa City kutolewa nje akiwa kwenye machela.

Man City tayari walikuwa wakiongoza wakati huo kupitia Sergio Aguero lakini Gabriel Jesus na mchezaji Leroy Sane aliyetokea bench wote wawili wakatupia mara mbili kila mmoja.

Comments

comments