Kutoka Bungeni: Huu ndio undani wa Tukio zima la Mhe. Lissu kupigwa risasi jana.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai, ametoa taarifa ya kina kuhusu tukio zima la kupigwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA Mh. Tundu Antiphas Lissu.

Bunge limetoa taarifa kupitia akaunti yake rasmi ya mtandao wa twitter, huku likisema kuwa Mhe. Lissu alipigwa jumla ya risasi tano na watu wasiojulikana kisha watu hao kukimbia.

Hivi sasa mbunge huyo yupo nchini Kenya kwenye hospitali ya Aga Khan iliyopo jijini Nairobi akipatiwa matibabu.

Comments

comments