Tundu Lissu apigwa risasi na watu wasiojulikana Dodoma

Taarifa zilizotufikia zinasema Mbunge wa Singida Mashariki, ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu amepigwa risasi akiwa Dodoma.

Tairi la mbele la gari linalodaiwa kuwa la Tundu Lissu na alama zinazodaiwa kuwa za risasi zilizopigwa kwenye kioo, kama  zinavyoonekana.

Aidha mbunge huyo amekimbizwa kwenye hospitali kuu ya mkoa kwa ajili ya huduma ya kwanza na matibabu.

Tutaendelea kukujuza kinachoendelea.

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe akiwa na mtu mmoja aliyebeba nguo zinazoaminika kuwa Tundu Lissu alizivaa kabla ya kushambuliwa.

Comments

comments