Hii hapa ratiba yote ya VPL wikendi hii

Mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara unatarajiwa kuendelea tena mwishoni mwa wiki hii, ambapo siku ya Jumamosi kutakuwa na michezo miwili na Jumapili Septemba 10 kutakuwa na michezo sita.

Ligi hiyo ilisimama ili kupisha mechi za kimataifa za kufuzu kucheza kombe la Dunia mwakani nchini Urusi, na kwa zile timu zisizogombea kushiriki kombe hilo, zilicheza michezo ya kirafiki na Tanzania nilicheza kirafiki dhidi ya Botswana na kushinda 2-0.

Mabingwa watetezi Dar Young Africans watakuwa mjini Njombe siku ya jumapili watakapo karibishwa na Njombe mji, huku vinara wa ligi Simba SC watacheza jumamosi dhidi ya Azam FC.

Ratiba kamili ni kama inavyosomeka hapa chini.

Comments

comments