Ronaldo awataja anaowahofia kumpiku Ballon d Or

Cristiano Ronaldo amewataja wapinzani wake anaodhani watatoa upinzani mkali kwake kwenye kuwania tuzo ya Ballon d’Or 2017, straika huyo wa Ureno alipendekeza wachezaji wanne ambao wanastahili tuzo hiyo.

Mshambuliaji huyo anayekipiga klabu ya Real Madrid anaamini kuwa ushindani wa tuzo hiyo ni kati ya wachezaji wanne, alisema ni Lionel Messi, Neymar, Robert Lewandoski na Gonzalo Higuain kama mpinzani wake mkuu wa tuzo.

Ronaldo alishinda tuzo hiyo mwaka 2016 wakati alipomshinda Lionel Messi na baadae kutwaa tuzo bora ya Wachezaji wa FIFA baada ya kushinda michuano ya Ulaya.

Comments

comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *