Picha za Stars ilipogonga mwamba kwa Chipolopolo

Timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars imeshindwa kuendeleza wimbi la ushindi kwenye michuano ya COSAFA Castle Cup inayoendelea nchini Afrika kusini baada ya kufungwa 4-2 na timu ya taifa ya Zambia (Chipolopolo).

Mchezo huo wa hatua ya nusu fainali ulipigwa jioni ya leo katika dimba la Maruleng ambapo Tanzania ndio iliyokuwa ya kwanza kupata bao kupitia Erasto Nyoni kabla ya wazambia kufunga goli mbili na kwenda mapumziko tukiwa nyuma.
Hadi filimbi ya Mwisho inalia, magoli ya Shonga 47′ na 68′ , Chirwa 53′ na Mwila 44′ kwa upande wa Zambia yaliweza kuamua ushindi wa mechi hiyo na kufuta ndoto za watanzania kutinga kwenye fainali.

Comments

comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *