Rais Magufuli atoa agizo la kusitisha utoaji wa leseni za kuchimba madini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo ameiagiza Wizara ya Nishati na Madini kusitisha utoaji wa leseni mpya za uchimbaji na halikadhalika leseni ambazo zimeisha muda wake. Ametoa maagizo hayo alipokuwa akizungumza na wananchi wa Geita ambao walizuia msafara wake katika maeneo mbalimbali wakati akiwa njiani kuelekea Chato.

Mapema kabla, Mheshimiwa Rais alihitimisha ziara yake ya kikazi ya Siku Mbili Mkoani Mwanza kwa kuzindua  mradi wa  Uboreshaji wa huduma ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira katika kijiji cha Nyamazugo Wilayani Sengerema.
Mradi huo wa maji umetekelezwa chini ya mpango wa maji wa Kamisheni ya Bonde la Ziwa Victoria ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa gharama ya shilingi bilioni 22.4. Mradi wa Maji Safi mjini Sengerema ulioanza tangu mwaka 2011 unatarajiwa kuwahudumia wakazi 138,000 ifikapo mwaka 2030.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Mradi huo, Mhe. Rais Dkt. Magufuli amesema kukamilika kwa mradi huo kutamaliza tatizo la maji la muda mrefu kwa wakazi wa Sengerema na maeneo ya jirani.
Mhe. Rais Dkt. Magufuli amewataka wananchi wanaozunguka mradi huo kuutunza na kuhakikisha hawaharibu vyanzo vya maji katika eneo hilo la ziwa Victoria ikiwa ni pamoja na kuacha uvuvi haramu ambao umekuwa na madhara makubwa kwa wananchi.

Comments

comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *