Cheki basi la Singida UTD

Singida United iliyopanda daraja msimu huu imeendelea kuonyesha kuwa inataka kuwa moja ya klabu za mfano hapa nchini hii ni baada ya leo Jumatatu kutambulisha basi lao jipya ambalo itakuwa ikilitumia kwa safari zake mbalimbali za michezo ya ligi kuu bara na ile ya kombe la shirikisho.

Utambulisho wa basi hilo lenye thamani ya Shilingi Milioni 330 umefanyika kwenye hoteli ya Lamada iliyopo Ilala jijini Dar Es Salaam na kushuhudiwa na waandishi wa habari toka vyombo mbalimbali.

Comments

comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *