Roma Mkatoliki akamatwa na watu wasiojulikana

Msanii Roma Mkatoliki amekamatwa usiku wa kuamkia leo akiwa studio za Tongwe Records jijini Dar es Salaam.
Msanii mwenzake Professor Jay ambaye ni mbunge wa jimbo la Mikumi kupitia ukurasa wake wa instagram amesema kuwa
“Nimestushwa sana kusikia kuwa kuna watu wamevamia studio za TONGWE RECORDS majira ya saa moja usiku na wamemchukua ROMA @roma2030 , MONI @moni_centrozone na kijana wa Kazi na pia wamechukua COMPUTER ya studio na Screen (Tv) na wameondoka navyo kusikojulikana..
Mpaka sasa hatujui wamewapeleka wapi!!”
Taarifa zaidi tutaendelea kukusogezea, tafadhali endelea kuwa karibu nasi.

Comments

comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *