Nay wa mitego atangaza maisha yake yapo hatarini

Siku chache baada ya rapa Nay wa mitego kukamatwa na polisi akiwa mjini Morogoro, kisha kusafirishwa hadi jijini Dar Es Salaam na baadae kuachiwa huru kwa amri ya rais, Msanii huyo kupitia ukurasa wake wa instagram amepost maneno yanashitua ambapo yanaashiria maisha yake yapo hatarini.
Ujumbe huo ulisomeka
“Usalama wa Maisha yangu umekua Mdogo kwasasa, Wana panga kunipoteza ikibidi nisiwepo kabisa kwenye hii Dunia. Nipo tayari kwa chochote wanacho panga kufanya Coz sijajipanga kupambana nao, Mimi ni Mwana Muziki si vingine. Kwa chochote kitachotokea Familia yangu itakua na chakuongea. Siwezi kuhama Nchi wala kukimbia nitafia hapa hapa. Na siko tayari kupindisha Chochote.! Nyie Ndo mtanilinda. Sina Mlinzi na sitarajii kua na mlinzi. OnlyGod
#Wapo
#Truth”
Tunafanya juhudi za kumpata aweze kutuambia kwa undani kulikoni hadi amefikia huku.

Comments

comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *