Mishahara tatizo Simba SC

Wachezaji wamepoteza ari ya kujituma wawapo uwanjani na hiyo imechangiwa na kucheweleshewa mishahara yao

Nahodha wa klabu ya Simba Jonas Mkude, amesema sababu ya timu yao kushindwa kuonyesha kiwango cha kuvutia katika mechi mbili zilizopita ni kutokana na kutolipwa mishahara yao ya miezi miwili.
Mkude ameiambia Goal,  asilimia kubwa ya wachezaji wamepoteza ari ya kujituma wawapo uwanjani na hiyo imechangiwa na kucheweleshewa mishahara yao.
“Unajua wachezaji nao wana majukumu yao binfasi na wanafamilia zinawategemea sasa unapomcheweleshea mshahara wake tena kwa miezi miwili unadhani ataishije hata huo moyo wa kucheza kwa kujituma utatoka wapi ni vyema uongozi ukatambua kama hii ni kazi na wanapaswa kutujali,” amesema Mkude.
Nahodha huyo amebaye hivi karibuni alikuwa na malumbani na uongozi wa timu yake amesema kipindi hiki uongozicunatakiwa kuwa makini kwa kutimiza kila kitu kwa wachezaji na benchi la ufundi kwasababu ligi inaelekea mwishoni ili kumpata bingwa hivyo endapo watawavunja nguvu wachezaji itakuwa ngumu kutwaa ubingwa kama ambavyo wamekusudia.
Mkude amesema kwaxnafasicwaliyopo kwenye msimamo wa Ligi hawapaswi kuchanganyana na uongozi hasa katika mambo ya mishahara kwasababu endapo watalegea kidogo apinzani wao Yanga wanaweZa kuwapiku na kurudi kwenye uongozi wa Ligi na haitakua rahisi kuwatoka.
“Viongozi wenyewe anatambua vita ya ubingwa iliyopo Kati yetu na Yanga alafu leo unamcheweleshea mshahara mtu ambaye ndiyo mpambanaji uwanjani siyo sawa kwakweli hakuna mtu ambaye anaweza kucheza kwa nguvu wakati familia yake haina chakula au yeye mwenyewe hujala,” amesema Mkude.
Simba wanaoshika nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa Ligi ya Vodacom kesho w anaingia kambini kujiandaa na mcheso wao as ligi hiyo utakapokuwa Januari 29 uwanja wa Uhuru dhidi ya Azam FC

Goal.com

Comments

comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *