Show ya Beyonce yaahirishwa kupumzisha koo

Kampuni iliyokuwa imeandaa show ya mwanadada Beyonce ambayo ilibidi ifanyike kesho Jumatano huko New Jersey nchini Marekani imetangaza kuahirisha onesho hilo kwa sababu daktari wa mwanamuziki ametaka apumzishe koo baada ya kufanya show kibao.

Beyonce akiwa anatumbuiza (picha kwa hisani E news)
Show hiyo sasa imesogezwa mbele hadi tarehe 7 mwezi ujao, lakini show zingine zilizokuwa zimepangwa kupigwa St. Louis, Los Angeles, Santa Clara, Houston, New Orleans, Atlanta, Philadelphia na Nashville zitaendelea kama ilivyopangwa, na tayari waandaaji wameomba radhi ya katizo hilo kupitia taarifa waliyoitoa.

Beyonce ambaye Septemba 4 mwaka huu alitimiza miaka 35, hajazungumza chochote kuhusu taarifa hizo na amebakiza matamasha tisa anayotakiwa ayafanye kwenye tour yake ya Formation World.


Comments

comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *